Rais wa Argentina
Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa
lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la
kimataifa.
Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake
kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku
akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya Penalti. ''Amemwita
na kumueleza namna anavyoona fahari kwa kiwango kizuri kilichoonyeshwa
na timu yake katika michuano hiyo huku akimtaka asisikilize maneno ya
watu'' ilisema msemaji wa Rais Macri. Ndani ya miaka mitatu Messi
ametinga katika fainali tatu tofauti moja ikiwa ni ya kombe la dunia
nchini Brazili mwaka 2014 ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani,na
nyingine mbili za Copa America moja ikiwa mwaka 2015 na 2016 zote timu
yake ikipoteza dhidi ya Chile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment