0

Simba watatu ambao wanalaumiwa kwa kuwaua watu kadha mashariki mwa India watazuiliwa maisha yao yote.

Simba hao mmoja wa kiume na wawili wa kike, walikuwa wakiishi katika jimbo la Gujarat, wakati watu watatu wakiwemo mtoto wa kiume ,waliuwa katika visa tofauti miezi ya hivi karibuni

Maoafisa wanasema kuwa watu hao waliuawa na simba na kiume huku wale wa kike wakirarua miili yao.

Simba wa kiume atapelekwa kwa bustani ya wanyama huku wale wa kike wakipelekwa katika hifadhi ya kuwatunza wanyama.

Post a Comment

 
Top