Baada ya
baadhi ya wabunge wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge
kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge.
Leo June
17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Spika,
Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge
wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.
Mbunge
Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge
baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua
magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari
inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Licha ya
Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya
bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo
anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.
Aidha
Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya
bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba
William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam.
Post a Comment