Takriban maafisa
302 wa polisi wamefutwa kazi nchini Kenya kwa kukataa kukaguliwa tangu
mpango huo wa kutaka kukabiliana na ufisadi kuanzishwa mwaka
2013,kulingana na tume inayotekeleza ukaguzi huo.
Hayo
yalibainishwa na Jonhston Kavuludi ,anayeongoza tume hiyo ya huduma za
maafisa wa polisi huku maafisa wa polisi wakijiandaa kuhojiwa na jopo
katika mji wa magharibi wa Kisumu.
Ukaguzi huo ni mpango wa uma na
hufanywa mbele ya kamera ambapo maafisa uhojiwa kuhusu mali na fedha
wanazomiliki huku mgongano wowote wa maslahi ukichunguzwa.
Mwezi
uliopita wakati jopo hilo lilipokuwa Mombasa ,afisa mmoja wa idara ya
trafiki hakuweza kusema ni wapi alipata takriban dola 500,000 ambazo
ziliwekwa katika mtandao wa simu unaotuma fedha ama kupokea na akaunti
yake ya benki.
Wakenya katika mitandao ya kijamii walishangazwa na
kuelezea vile wanavyolazimishwa kutoa hongo baada ya kukamatwa kwa
makosa ya trafiki.
Post a Comment