0

Memphis Depay

Kiungo Mholanzi Memphis Depay hana uhakika kama ataendelea kubaki katika kikosi cha Manchester United chini ya Kocha mpya, Jose Mourinho.
 
 Depay ameanza kuhamisha vita vyake kurudisha kwao nchini Uholanzi akianza na magari yake ya kifahari.

Gari lake la kifahari aina ya Mercedes G Wagon lenye thamani ya pauni 100,000 pamoja na pikipiki aina ya Scorpion yenye thamani ya pauni 13,500 pia zimepelekwa kwao Uholanzi.

Tayari kuna taarifa Mholanzi huyo mwenye miaka 22, alianza kusafirisha gari lake la kifahari zaidi aina ya Rolls Royce Wraith lenye thamani ya pauni 250,000 kulirejesha kwao Uholanzi. Hata hivyo, bado Mourinho bado hajatoa Orodha ya wachezaji watakaobakia au kuondoka clabuni hapo.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top