0


Dar es Salaam.  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imesema ili kuinusuru Serikali na tatizo la watumishi hewa itahakikisha ifikapo Desemba 31 kila mwananchi atakuwa amepata kitambulisho ili kisaidie utambuzi.

Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce Malibicho alisema jana kuwa vitambulisho hivyo vitasaidia kukabiliana na tatizo hilo.

Hatua hiyo inakuja wakati Serikali ikihaha kung’amua watumishi hewa wanaotafuna mishahara bila kufanya kazi.

Mkurugenzi huyo alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), tayari imetoa mchango wao wa vifaa vitakavyofanikisha usajili unaotarajia kuanza hivi karibuni mikoa yote nchini.

Post a Comment

 
Top