0

Zikiwa zimebaki siku mbili tu ambapo kwa wale wa ughaibuni wanasema 'Two days to go' ili kuanza kwa Mashindano yenye mvuto wa aina yake na utamu wa kabumbu lenye ufundi na vipaji vya hali ya juu toka Bara la Amerika ya kusini. Leo katika mfululizo wa kuelekea michuano hii tunaangazia timu shiriki,makundi yao na wasifu wa baadhi ya timu.

Timu zitakazo shiriki michuano hii maalumu ya kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ni timu 16, ambapo timu 10 ni wanachama wa shirikisho la kabumbu la Amerika ya Kusini (CONEMBOL) na timu 6 ni waalikwa ambazo zote zinatoka shirikisho la kabumbu la Amerika ya kati na kaskazini (CONCACAF). Nchi hizo 16 ni Argentina, Brazil, Bolivia, Chile, Colombia, Equador, Paraguay, Peru, Uruguay na Venezuela (CONEMBOL). Costa Rica, Haiti, Jamaica, Mexico, Marekani na Panama (CONCACAF).

Timu hizi zimegawanywa katika makundi manne yenye timu nne kila kundi, ambapo michezo hiyo itachezwa kwenye viwanja vya mji kumi tofauti nchin Marekani. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-

CHILE

Hawa ndiyo wanaolitetea taji lao walilolitwa mwaka jana 2015, Chile wanajivunia wachezaji kama mshambuliaji Alexis Sanchez, mshambuliaji mwenye nguvu na kasi anayefanya vizuri kwenye EPL akiwa na klabu ya Asernal. Pia watamtegemea sana kiungo wao mtukutu lakini makini sana awapo uwanjani, huyu ni Artulo Vidal, huyu ndiyo muhimili wa timu kwani huwa na jukumu kubwa la kuunganisha timu. Tegemeo lao jingine ni kwa golikipa wao Claudio Bravo anayekipiga kwenye klabu ya Barcelona ya nchini Hispania. Swali ni je watalitetea taji lao hasa baada ya kuachana na kocha aliyewapa mafanikio makubwa pamoja na taji hilo JORGE SAMPAOLI?

URUGUAY

Hawa ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hii kwani wao wameweza kuchukuwa taji hilo mara nyingi kuliko timu yoyote ya ukanda huo. Chini ya kocha OSCAR TABAREZ, Uruguay watamtegemea sana mshambulizi anayesukuma ndinga katika timu ya PSG nchini Ufaransa Edson Cavani kufuatia kuumia kwa mshambuliaji nguli kabisa aliyechukuwa kiatu cha ufungaji bora kwenye Laliga Luis Suarez. Katika idara ya ulinzi watamtegemea zaidi Diego Godini, mlinzi mwenye roho ya paka anayepambana mpaka dakika ya mwisho.Mchezaji mwingine wa kuangaliwa katika kiosi hiki ni Max Perreira.

BRAZIL

Brazil wanaonekana kutoipa umuhimu mkubwa sana michuano hii bali wataelekeza nguvu kwenye michuano ya Olimpiki itakayo fanyika nchi humo baadaye mwaka huu, hii inatokana na kuwaacha nyota wake wengi kama Oscar, Thiago Silva,David Luiz na mshambuliaji matata Neymar wakisema wazi kuwa hao wote watashiriki kwenye michezo ya olimpiki. Sasa kazi kubwa kwa kocha Carlos Dunga ni namna atakavyo watumia wachezaji machachali kama F.Coutinho wa Liverpool, mlinzi Dani Alves, mkongwe Ricardo Kaka mshambuliaji mwenye nguvu Hulk na wengineo chipukizi.

ARGENTINA

Sijui mfumo gani atakaoutumia kocha GERARD MARTINO katika mashindano haya hasa kutokana na hazina kubwa ya wachezaji alionao kikosini, ingawa tunategemea kuona wachezaji wa Argentina watacheza wakimzunguka gwiji wa wakati huu mchezaji bora wa dunia mara tano Lionel Messi. Katika ushambuliaji Messi ataanza na nani kati ya Gonzalo Higuaini au Sergio Aguero na nyuma yao kutokea pembeni wakiunganishwa na A.Di Maria na ukutwa utakaoongozwa na Nicolas Otamendi.

Post a Comment

 
Top