Michuano ya Copa
America imefikia tamati leo hii kwa mabingwa watetezi Chile kuendeleza
ubabe wake dhidi ya Vigogo wa soka duniani Argentina.
Dakika 120
za mchezo huo zilishuhudia timu hizo zikienda suluhu ya bila kufungana.
Mchezo huo ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku ikushuhudiwa timu
zote mbili zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji 10 baada ya
Marcelo Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu
dakika ya 28 kabla ya Marcos Rojo wa Argentina kutolewa nje dakika ya 43
kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja. Katika upigaji wa penalti,Arturo
Vidal wa Chile alianza kwa kukosa kabla ya Lionel Messi na Lucas Biglia
kukosa kwa upande wa Argentina. Hii inakuwa fainali ya pili ndani ya
miaka miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua ya fainali amapo
mara zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju ya penalti.
Fainali hizi zilichezwa mwaka jana nchini Chile na kurudiwa mwaka huu
ikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tokea kuanza kwa michuano hii mwaka
1916.
Post a Comment