Chama cha upinzani
nchini Tanzania CHADEMA kimesema kuwa kitaenda mahakamani kupinga
tangazo la hivi karibuni la polisi kwamba mikutano yote ya hadhara
inyofanywa na upinzani imepigwa marufuku.
Kulingana na gazeti la
Citizen nchini Tanzania, uamuzi huo wa kwenda mahakamani ulitangazwa na
naibu katibu mkuu wa CHADEMA Saumu Mwalimu huko Mwanza.
Inajiri baada ya mkutano wa siku mbili wa maafisa wakuu wa upinzani wakiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa Freeman Mbowe.
Gazeti
hilo limesema kuwa maafisa wa Chadema na wabunge kadhaa wako katika mji
huo wa Ziwa baada ya kuzuiliwa kufanya mkutano katika eneo la Kahama
siku mbili zilizopita.
Maafisa wa polisi walisema kuwa mkutano huo
ulioshirikisha chama cha ACT-wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa
kigoma Zitto Kabwe utapigwa marufuku.
Na siku ya Ijumaa Bw Malimu
amesema kuwa watawasilisha kesi ya kutaka kubadilisha uamuzi huo wa
polisi katika mahakama kuu Mwanza.
Post a Comment