Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Africa Mashariki inawataka wafanyabiashara nchini Tanzania kuchangamkia fursa za kibiashara zinazopatikana katika soko la pamoja la nchi wanachama wa afrika Mashariki ambapo kwa hivi sasa hawatatozwa ushuru wa forodha.
Akiongea hii leo na mkuu wa kitengo cha habari wa wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Mindi Kasiga amesema kuwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki hivi sasa wanauhuru wa kufanya biashara bila ya kulipa ushuru wa forodha kwa sharti moja tuu la bidhaa zao kuwa zimekidhi vigezo vya ubora na kufuata utaratibu ulioanishwa.
Kwa wafanyabiashara wanaotaka kufanya biashara zao nchini Sudan ya Kusini Bi Mindi amesema kuwa bado utaratibu wa kufanyabiasahara huko haujakamilika kufuatia nchi hiyo kujiunga na jumuiya muda wa hivi karibuni na itaruhusiwa kufanaya biashara ya pamoja endapo itarejesha hati ya kujiunga na jumuiya.
Post a Comment