Klabu ya Barcelona
imekubali kulipa faini ya euro milioni 5.5 kutokana na makosa
waliyofanya katika ulipaji kodi kufuatia usajili wa Neymar kutoka Santos
mwaka 2013.
Waendesha mashitaka wa Uhispania walikuwa wakiituhumu Klabu hiyo kwa kuficha thamani halisi ya manunuzi ya mchezaji huyo.
Barcelona
ilitangaza kulipa ada ya euro milioni 57, huku euro milioni 17 zikienda
kwa klabu yake ya Santos na zilizobakia zikienda kwa wazazi wa Neymar.
Lakini
kampuni moja ya uwekezaji ya Brazil ambayo ilikuwa ikimiliki haki za
asilimia 40 za Neymar ilidai hawajalipwa kiasi stahiki huku wachunguzi
wakieleza kuwa gharama halisi walizolipa Barcelona ni euro milioni 83.
Hata
hivyo, mabingwa hao wa Uhispania sasa wamepata suluhu ya tatizo hilo
kwa kuamua kulipa faini kutokana na makosa yaliyofanyika.
Post a Comment