Copa Amerika hii nayo habari nyingine ya
mjini kimichezo itakayoanza usiku wa Jumamosi kwa saa za Afrika
Mashariki, ni michuano inayokuwa na msisimko wa hali ya juu japo kwa
Bara la Afrika hawana ganzi nayo sanaa. Michuano hii ilianzishwa mwaka
1916 wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.
HISTORIA FUPI YA COPA AMERIKA
Michuano hii ina miaka 100 sasa, tayari
imetimiza karne 1 tangu ianzishwe, na michuano ambayo inatoa vipaji
vingi vitakavyokuja kucheza Ulaya. Inashirikisha timu 16 hatua ya
makundi zinapangwa timu nne na makundi yanakuwa manne.
KWANINI IMEFANYIKA MARA MBILI MFULULIZO?
Bingwa mtetezi ni Chile, kwa mara ya
kwanza tangu michuano hii ianzishwe imefanyika mwaka jana na mwaka huu
inatimiza miaka 100. Kwa heshima ya miaka 100 au karne moja ndio
wameamua ifanyike tena mwaka huu. Ila kwa kawaida hufanyika kila baada
ya miaka 3 baada ya mwaka huu itafanyika tena 2019.
Bingwa wa kihistoria wa michuano hiyo ni
URUGUAY amechukua mara 15 huku ECUADOR na Venezuela ikiwa bado
hawajachukua michuano hiyo. Wachezaji nyota kutoka Ligi za mataifa ya
Ulaya kama England, Spain, Ufaransa na Italia wote wapo huku.
Hii ndio Copa America, South America Football Championship ama Kihispania wanaita Componet Sydamericano De Futbol.
Post a Comment