0


Mchezo uliovutiwa na mashabiki wengi kutokana na timu zote za leo zikiwa na hostoria ya kupoteza michezo yake

Ligi ya mbuzi Vijana Cup imeendelea tena hii leo katika mchezo mmoja uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi muungano Wilayani Liwale kati ya Nangando fc dhidi ya Zfc na   umemalizika kwa Zfc kuibuka na ushindi wa goli 3-2.

Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wakusisimua Nangando fc  ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Shadhili lihambamba katika dakika ya 22 goli lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 50 Z fc walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Mustafa Malunda lakini dakika tano baadae Nangando walipata goli la pili kupitia kwa Fadhili Mbwana mnamo dakika ya 70 Z fc walipata goli la kusawazisha kupitia kwa Mussa kisanga lakini Yahaya likule akamalizia msumali wa mwisho baada ya kuifungia Z fc goli la ushindi katika dakika ya 82.

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Nangando Abduli ngeta  alisema wachezaji wake wamejituma lakini mpira ni mchezo wa makosa na bahati haikuwa kwao ndio maana wamepoteza mechi ya leo pia alimeji matumaini ya kushindi kwa mechi ijayo.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo kati ya Sido Fc dhidi ya Black stars

Post a Comment

 
Top