Aliyekuwa winga wa
timu ya Ufaransa David Ginola anaendelea kupata afueni hospilini mjini
Monaco baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mchezaji huo mwenye
umri wa miaka 49 ambaye aliwahi kuichezea Newcastle,Tottenham,Aston
Villa an ambaye alijiuzulu mwaka 2002 alianguka na kuzirai kusini mwa
Ufaransa.
Daktari aliyemfanyia upasuaji huo amesema kuwa Ginola alinusurika kifo.
Ujumbe
wa Twitter kutoka kwa nyota huyo wa zamani ulisema: Walimwengu
hamjambo,sikulala vizuri.Niko salama ,ijapokuwa nataka kupumzika kiasi.
David
alicheza katika mechi ya hisani .Lakini ghafla akaanguka na kuzirai
huku watu wakidhani ilikuwa mzaha lakini baada ya dakika mbili wakabaini
mchezaji huyo yupo hatarani,alisema Gilles Dreyfus,profesa wa upasuaji
katika hospitali ya kukabiliana na magonjwa ya moyo huko Monaco.
Post a Comment