0

Ligi ya mbuzi vijana cup-wilayani Liwale iliendelea tena jana mei 22 kwa mchezo mmoja kati ya kati ya Black star dhidi ya Wakaanga Sumu.

Lakini timu ya Black star haikujitokeza uwanjani na haijatoa taarifa yeyote kwa uongozi wa Ligi .
Uongozi wa ligi unalazimika kutoa pointi tatu kwa timu ya Wakaanga Sumu kupewa ushindi wa goli tatu   na point 3.
Timu ya Black star katika hatua ya makundi imeanza vibaya baada ya kupoteza mechi nne zote za mwanzo na jana ilikuwa wamaliza ndipo  maana hawajajitokeza uwanjani kukamilisha mchezo wao dhidi ya Wakaanga Sumu.
Leo mei 23 kutakuwa na mchezo kati ya Kigamboni fc Vs Mnalani fc mchezo utakao timua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano.

Mchezo wa kesho unatarajia kuwa mchezo wa mkali kwakuwa Kigamboni wanataka kuendeleza kuweka rekodi ya kutokupoteza mchezo wowote katika Ligi.

Post a Comment

 
Top