|
WABUNGE
wameitaka serikali kuweka mkazo katika kuhakikisha ardhi yote nchini
inapimwa. Pia, wametaka kuwepo na programu ya kupima ardhi nchi nzima na
kuwauzia wananchi, jambo litakalosaidia kuondoa migogoro ya ardhi.
Wametaka
suala la upimaji kutoachwa kwa sekta binafsi, ambayo kwa mujibu wa
wabunge, ina gharama kubwa; badala yake, serikali ijiwekee mkakati wa
kupima angalau mikoa miwili kila mwaka.
Aidha,
wabunge wameyashukia mabaraza ya ardhi huku wakikosoa kutumia watu wasio
na taaluma ya sheria katika kuamua kesi. Walitoa maoni hayo jana wakati
wakichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi.
Walisisitiza
umuhimu wananchi kupimiwa ardhi na kupatiwa hati. Walia upimaji ardhi
Mbunge wa Mbinga, Sixtus Mapunda (CCM), alisema kuwe na programu maalumu
ambayo serikali itakuwa na vifaa vya upimaji nchi nzima na kupima ardhi
yote ; na pale mwananchi anaponunua ardhi anakuta eneo limepangwa.
Alisema
hatua hiyo itasaidia kuondoa usumbufu wa kupima kwa gharama kubwa na
wakati huo huo kukabili migogoro ya ardhi. Alitoa mfano wa Jiji la Dar
es Salaam, ambalo serikali inakabiliwa na usumbufu wa kulipanga.
Mbunge wa
Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba (CCM) aliunga mkono umuhimu wa
kupima maeneo yote, kuondoa utata na kumaliza migogoro ya ardhi.
Mwingine aliyehimiza upimaji wa maeneo yote ni Mbunge wa Viti Maalumu,
Cecilia Paresso (Chadema ) ambaye alishauri wananchi wapimiwe maeneo kwa
kuwakopesha kisha walipe madeni hayo taratibu.
Alisema
kwa kufanya hivyo serikali mbali na kuondoa migogoro ya ardhi, pia
itaingiza kipato kutokana na wananchi kulipia hati. Wakosoa mabaraza
Wakati huo huo katika kuchangia, baadhi ya wabunge wametaka kazi za
kiutendaji katika masuala ya ardhi zifanywe na wataalamu wa ardhi ; na
serikali iachane na utaratibu wa sasa wa kuwapa kazi watu kiholela.
Walitaka
mabaraza ya ardhi yasimamiwe na wataalamu wa ardhi, badala ya kuchukua
watu wasio na taaluma. Mbunge wa Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka (CCM),
alieleza kushangazwa na kitendo cha serikali kukabidhi jukumu kubwa la
usuluhishi wa masuala ya ardhi kwa watu ambao hawajasoma na hawajui
sheria za ardhi.
Alisema,
wapo wataalamu wengi nchini ambao wamekwenda kusomea masuala ya ardhi
wanaotakiwa kufanya kazi hiyo, lakini wamekuwa wakitumiwa watu maarufu
vijijini kufanya kazi hiyo.
Post a Comment