
- 1.0.UTANGULIZI
Kwa
kipindi cha kuanzia Januari 1, 2016 hadi kufikia Machi 31, 2016 ofisi
ya TAKUKURU (M) LINDI imetekeleza majukumu yake ambayo kimsingi
yamegawanyika katika makundi makuu matatu ambayo; ni Uchunguzi, Elimu
kwa Umma na Utafiti, Udhibiti na Takwimu kama ifuatavyo:-
- 2.0.UCHUNGUZI
Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI imetekeleza kazi za uchunguzi kama ifuatavyo:-
- 2.1.Idadi ya Taarifa zilizopokelewa
Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI imepokea jumla ya taarifa Arobaini namoja (41) za vitendo vya Rushwa kwa kipindi cha kuanzia Januari 1, 2016 hadi Machi 31, 2016,katika idara ya AFYA -13, TAMISEMI(Serikali za mitaa) – 9,ARDHI - 8,USHIRIKA – 5,KILIMO -3,MAHAKMA -1,ELIMU -1,UJENZI -1 na MALIASILI – 1.
Kutokana
na taarifa hizi hadi sasa tumefungua majalada saba (7) ambayo yapo
katika hatua mbalimbali za uchunguzi aidha majalada haya yanahusiana
zaidi na idara ya Afya hasa katika fedha za wafadhili (BASKET FUND,EGPAF na TASAF)
- 2.2.Idara zinazoongoza kwa kulalamikiwa
Kufuatia
taarifa za vitendo vya rushwa zilizopokelewa katika ofisi ya TAKUKURU
(M) LINDI, Idara zinazoongoza kwa kulalamikiwa ni pamoja na Idara ya AFYA, TAMISEMI ARDHI na USHIRIKA.
- 2.3.Idadi ya kesi zilizofikishwa Mahakamani
Kwa kipindi cha kuanzia Januari 1, 2016 hadi Machi 31, 2016 ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI imefikisha na kufungua kesi saba (7)
mpya Mahakamani. Kesi hizi zimefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu
mkazi Lindi- 1,Mahakama ya Wilaya ya Kilwa - 4 na Nachingweha - 2.
- 2.4.Idadi ya kesi zinazoendelea Mahakamani
Kwa kipindi hicho hicho cha kuanzia Januari 1, 2016 hadi Machi 31, 2016 ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI inajumla ya kesi ishirini na tisa (29)
zinazoendelea Mahakamani. Kesi hizi zote zinaendeshwa katika Mahakama
ya Hakimu mkazi Lindi - 5,Mahakama ya Wilaya ya Liwale - 6,Nachingwea -
3,Kilwa -13 na Ruangwa - 2.
- 2.5.Thamani ya Fedha/Mali iliyookolewa
Ofisi
ya TAKUKURU (M) LINDI imefanikiwa kuokoa jumla ya Tshs. 735,000/-
zilizokuwa zimelipwa kwa watumishi wa Idara ya Afya Wilaya ya Liwale
kama posho ya safari za kazi ambazo kazi ya malipo hayo haikufanyika.
Posho hizo zilirejeshwa na watumishi wa idara hiyo baada ya uchunguzi
dhidi yao kuanzishwa aidha ofisi imeshauri wachukuliwe hatua za
kinidhamu na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Liwale.
- 3.0.ELIMU KWA UMMA
Kwa
kipindi cha kuanzia mwezi Januari 1, 2016 hadi Machi 31, 2016
uelimishaji umma juu ya vitendo vya rushwa na athari zake kwa jamii
umefanyika kama ifuatavyo:-
- 3.1.Semina
Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI kwa kipindi tajwa hapo juu imeendesha jumla ya Semina 43
kwa makundi mbali mbali ya jamii ambapo jumla ya wananchi 4354 wamepata
semina kati yao ME 2447 na KE 1907 wakiwemo viongozi wa tarafa, kata na
vijiji, waheshimiwa madiwani, watumishi wa idara ya afya, wachezaji,
makocha, viongozi na mashabiki wa timu za mpira wa miguu, wavuvi na
viongozi wao, madereva wa bodaboda na bajaji, wakulima, waratibu
wajasiriamali mbalimbali, wajumbe wa chama cha wabanguaji korosho,
viongozi wa bodi wa bodi za vyama vya msingi kwa Lengo la kuhamasisha na
kuelimisha llikuwa ni wahusika waweze kutoa taarifa za vitendo vya
rushwa, kuelewa majukumu yao na namna ya kushirikiana na TAKUKURU jinsi
ya kupambana na Rushwa.
- 3.2.Kufungua na Kuimarisha Klabu za wapinga rushwa
Kwa
kipindi cha kuanzia Januari 1, 2016 hadi Machi 31, 2016 ofisi ya
TAKUKURU (M) LINDI imefungua na kuimarisha Klabu za wapinga rushwa
katika shule za Sekondari na Msingi kama ifuatavyo:-
ü Shule za Sekondari: Jumla ya Klabu 41
zimetembelewa na kuimarishwa ikiwa ni pamoja na kutoa mwongozo kwa
wanachama wapya wa kidato cha kwanza na kidato cha tano, pia kuchagua
viongozi wa vilabu na kugawa majarida.
ü Shule za Msingi: Jumla ya Klabu 15
zimefunguliwa ikiwa ni pamoja na kusimika walimu walezi wa klabu hizo,
Pia kuongea na wanafunzi ili kuwajengea uadilifu tangu wakiwa wadogo.
Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI kwa kipindi tajwa hapo juu imefanya mikutano ya hadhara/mijadala ya wazi 17
kwa kuelimisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwatembelea
wafungwa na mahabusu, viongozi na wanachama wa vyama vya msingi,
wananchi mbalimbali waishio vijijini, watumishi katika mahakama ya
wilaya pamoja na wananchi waliohudhuria siku ya sheria duniani.
Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI kwa kipindi tajwa hapo juu imeandika makala mbili(2)
ü Usimamizi mbovu wa miradi ya maji vijijini ni sababu kuu ya wananchi kukosa maji safi na salama (W) Nachingwea.
ü Mianya ya Rushwa inayosababishwa na ukiukwaji wa sheria na mfumo wa manunuzi katika vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS).
- Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI kwa kipindi tajwa hapo juu imeshiriki katika shughuli mbalimbali za jamii,ambazo ni pamoja na
ü Usafi wa mazingira
ü Upandaji wa miti katika vyanzo vya maji
- 4.0.UTAFITI, UDHIBITI NA TAKWIMU
Kutokana
na taarifa tulizopokea kutoka kwa wananchi kwa kipindi cha kuanzia
mwezi Januari 1, 2016 hadi Machi 31, 2016 Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI
imefanya dhibiti kama ifuatavyo:-
- 4.1.Udhibiti
Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI imefanya dhibiti sita (6) katika Idara mbalimbali kama Ifuatavyo:-
- IDARA YA ARDHI
Uchambuzi
wa Mfumo kuhusiana na Mianya ya Rushwa katika Mradi wa Upimaji wa
Viwanja vya Makazi katika eneo la MLANDEGE – Kata ya NACHINGWEA.
- IDARA YA KILIMO NA USHIRIKA
Uchambuzi wa Mfumo wa Manunuzi katika AMCOS za MKOMBOZI, NAIPANGA NA NAMANJI katika H/W NACHINGWEA
- Pia kuhusiana na Mianya ya rushwa katika Mfumo wa Ununuaji wa pembejeo za korosho za ruzuku katika AMCOS ya NAMBALAPALA katika Halmashauri ya Wilaya ya NACHINGWEA.
- IDARA YA ELIMU
Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya LIWALE imefanya utafiti mdogo katika
Idara ya Elimu kufuatia kuwepo kwa baadhi ya walimu wakuu wa shule za
msingi kuendelea kuchangangisha michango kwa wazazi waliokuwa
wakiwaandikisha watoto wao kwa ajili ya kuanza darasa la kwanza Januari,
2016 kinyume na maelekezo ya WARAKA
WA ELIMU NA. 5 WA MWAKA 2015 wenye maelekezo ya KUFUTA ADA KWA ELIMU YA
SEKONDARI KIDATO CHA KWANZA MPAKA CHA NNE KWA SHULE ZA UMMA NA MICHANGO
YOTE KATIKA ELIMU YA MSINGI.
- IDARA YA MAJI
Ofisi
ya TAKUKURU Wilaya ya NACHINGWEA imefanya Udhibiti wa fedha za miradi
ya maji vijijini inayofadhiliwa na Benki ya Dunia katika Vijiji kumi vya
Halmashauri (W) NACHINGWEA.
- IDARA YA AFYA
Ofisi ya TAKUKURU (W) KILWA imefanya Uchambuzi wa Mfumo wa Ukusanyaji wa mapato katika Hospitali ya KINYONGA Wilaya ya KILWA.
- 4.2.Warsha
Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI imeandaa na kuendesha Warsha katika Idara mbalimbali kama Ifuatavyo:-
- IDARA YA ARDHI
Ofisi
ya TAKUKURU Mkoani imeendeshaWarsha ya wadau wakiwamo Watendaji wa
Mitaa na Kata, Afisa Utumishi, Afisa ardhi kujadili matokeo ya Utafiti
kuhusiana na Mianya ya Rushwa katika Mradi wa Upimaji wa Viwanja vya
Makazi katika eneo la MLANDEGE – Kata ya NACHINGWEA.
- IDARA YA ELIMU
Ofisi
ya TAKUKURU (W) LIWALE imefanya warsha ikihusisha Ofisi ya DED, ELIMU,
WAZAZI. Warsha hii inahusu kuwepo kwa baadhi ya walimu wakuu wa shule za
msingi kuendelea kuchangisha michango kwa wazazi waliokuwa
wakiwaandikisha watoto wao kwa ajili ya kuanza darasa la kwanza Januari,
2016. Uchangishaji wa michango hiyo ulikuwa unakiuka maelekezo ya WARAKA
WA ELIMU NA. 5 WA MWAKA 2015 wenye maelekezo ya KUFUTA ADA KWA ELIMU YA
SEKONDARI KIDATO CHA KWANZA MPAKA CHA NNE KWA SHULE ZA UMMA NA MICHANGO
YOTE KATIKA ELIMU YA MSINGI.
- 4.3.Ufuatiliaji
Ofisi
ya TAKUKURU (M) LINDI katika Ofisi yake ya Wilaya ya LIWALE imefanya
ufuatiliaji moja (1) katika idara ya Elimu ili kuhakikisha kwamba WARAKA
WA ELIMU NA. 5 WA MWAKA 2015 wenye maelekezo ya KUFUTA ADA KWA ELIMU YA
SEKONDARI KIDATO CHA KWANZA MPAKA CHA NNE KWA SHULE ZA UMMA NA MICHANGO
YOTE KATIKA ELIMU YA MSINGI unafuatwa kikamilifu.
- 4.4.Miradi ya Maendeleo
Ofisi ya TAKUKURU (M) Lindi imetembelea na kukagua miradi kumi na saba (17) kama ifuatavyo ni Mradi wa:-
- Ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi MLANDEGE yenye thamani ya Tsh 58,777,960/=.
- Mradi wa umwagiliaji katika eneo la MAVUJI wenye thamani ya Tsh 300,000,000/=, NGONGOWELE wenye thamani ya bilioni moja na zaidi, MATAWANGO wenye thamani ya Tsh 183,000,000/=.
- Mradi wa visima vya maji LIPUYU wenye thamani ya Tsh 373,395,806.06/=.
- Mradi wa FARM 8 wenye thamani ya Tsh 46,146,700.20/=,
- Mradi wa kisima cha maji LIKOTWA wenye thamani ya Tsh 310,937.681.40/=.
- Mradi wa ujenzi wa zahanati ya NANGURUKURU wenye thamani ya Tsh 234,000,000/=.
- Mradi wa nyumba ya mkurugenzi wa H/W KILWA wenye thamani ya Tsh 203,000,000/=.
- Mradi wa nyumba mbili za wakuu wa idara ya H/W KILWA zenye thanani ya Tsh 260,749,500/=
- Mradi wa nyumba ya afisa kilimo wenye thamani ya Tsh 45,843,800/=.
- Mradi wa ujenzi wa ward za hospitali ya RUANGWA zenye thamani ya Tsh 208,000,000/=.
- Mradi wa ujenzi wa zahanati kijiji cha KITANDI wenye thamani ya Tsh 30,000,000/=.
- Mradi wa kisima cha maji MBEKENYERA wenye thamani ya Tsh 23,000,000/= na miradi mbalimbali ya hospital ya KITOMANGA.
- 5.0.MKAKATI WA TAKUKURU (M) LINDI KUMALIZA KERO KWA WANANCHI HASA KWA MAENEO YALIYOONGOZA KWA KULALAMIKIWA
- 1.Ofisi ya TAKUKURU (M) LINDI imepanga kuanzisha dawati la kupokea na kusikiliza malalamiko ya wananchi wanaopata huduma za AFYA katika Hospitali ya Mkoa na Wilaya zote. Aidha dawati hilo litafunguliwa karibu na lango la kuingia/kutoka katika Hospitali hizo. Dawati hilo litakuwa linafunguliwa asubuhi na kufungwa baada ya saa za kazi kwa muda wa wiki moja. Baada ya muda wa kupokea malalamiko kumalizika, ofisi itachukua hatua zinazofaa kutatua kero zitakazolalamikiwa na wananchi.
- 2.Kufanya ufuatiliaji wa fedha za wafadhili(BASKET FUND,EGPAF NA UKIMWI) zinazotolewa kwenye Halmashauri zote za mkoa wa Lindi ili kuweka mfumo mzuri na wa uwazi wa matumizi ya fedha hizo
- 3.Tunategemea kutatua migogoro ya ardhi(viwanja) kwa kutumia viongozi wa serikali na viongozi wa dini kwani tatizo hili lipo kwenye jamii zaidi.
- 4.Tumepnga kutoa elimu kwa umma kwa kutumia gari la matangazo na flat screen ili kuweza kufikia wananchi wengi kwa haraka na kukusanya malalamiko yao ili yaweze kufanyiwa kazi kwa haraka
- 5.Kukutana na watendaji wote wa kata na vijiji kuwaeleza malalamiko ambayo yametolewa dhidi yao na kero wanazozisababisha kwa wananchi.
IMEANDALIWA NA,
STEVEN CHAMI
MKUU WA TAKUKURU (M) LINDI
11/4/2016
Post a Comment