SURA
YA KWANZA.
“Toka! Toka! Toka! Leo ndio mwisho
wenu. Tumewavumilia vya kutosha sasa basi, Basi!” Zilisika nje ya nyumba ya
Mzee Shabani Mlakwama. Sauti za ghadhabu zilizochanganyika na hisia kali
vinywani vya baadhi ya vijana katika kijiji cha Tangeni miongoni mwa vijana
waliofika kuumaliza utawala wa Mzee Shabani Mlamkwama kama walivyoamini kuwa
mwisho wake umefika.
Kelele nyingi zilisikika kama vile
watu wanapomkimbiza mwizi, kwa nia tu kukomesha hali ile.
Uchungu wa kila kijana uliongezeka maradufu, yote visa na matukio ya kutisha ya ndani ya kijiji chao. Vijana kupotea, vifo vya kukutatanisha vikihusishwa na mazingira ya kichawi tena wa kutisha sana. Muhusika wa yote akiwa Mzee Shabani na familia yake.

Tangia kuhamia kwake muda mfupi tu,
Tangeni ilikumbwa na balaa. Hali ilikuwa mbaya zaidi, matukio ya kutisha
yalitawala. Ushirikina wa hali ya juu, wanakijiji kupotea, mazao hayapatikani
shambani, kila ukionesha juhudi unaambulia robo tatu tu ndani ya hekari nzima.
Haijalishi iwe ya mahindi au mchele, tabu tu!
Suala hili liliwapa wakati mgumu
sana viongozi wa kijiji pamoja na wanakijiji wenyewe. Hapo sasa ndipo
walipoamua kutafuta suluhisho na nini chanzo cha yote hayo.
Waganga na waganguzi kutoka katika kila pembe ya kijiji walitafutwa ila waligonga mwamba. Hawakujua nini tatizo linalowatafuna watu wa Tangeni ila walichojua kuwa ni pazito na si pa masikhara, inahitaji mganga tofauti kabisa wa kutoka nje ya Tangeni. Hivyo juhudi za kumsaka mganga zilianza na kwa bahati nzuri walimpata Bwana Mzanzu Wa Wazanzu, kiboko ya wachawi katika kila pembe ya Dunia. Kupatikana kwa bwana huyo, kidogo ilileta matumaini ndani ya kijiji cha Tangeni.

Ujio wa Mzanzu wa Wazanzu, kiboko ya
wachawi ulikuwa si ujio wa masikhara ndani ya kijiji cha Tangeni. Kila
Mwanakijiji alipata habari zake wakiamini sasa tatizo linaweza kuwa bayana kila
Mwanakijiji akajua ninikinachokisibu kijiji chao.
Kuwasili kwa Mzanzu Wazanzu, kiboko
ya wachawi ndani ya kijiji ilikuwa tumaini jipya. Waliteuliwa vijana wachache,
kama kumi na wawili ilikuweza kumsaidia na kumpa mahitaji wakati wa shughuli
yake itakapoanza. Mzanzu aliagiza mahitaji yote ikiwemo mtama, uwele, ufuta,
pamoja na kondoo dume kwa ajili ya kazi hiyo ambayo alipanga kuifanya majira ya
saa saba za usiku wakati dunia ikiwa inajibadili kama waaminiavyo Wachawi
katika ulimwengu wa giza.
Vifaa vyote muhimu vilikamilika,
ilibakia muda wakuanza shughuli yake Mzanzu Wazanzu, kiboko ya wachawi. Muda
ulienda kwa kasi na hatimaye wakati wenyewe wa shughuli ulitimia.
Mzanzu Wazanzu akiongonzwa na wale
vijana kumi na wawili, aliaanza kazi huku akionesha kujiaamini kwa kiasi
kikubwa sana. Alichukua mtama, uwele, ufuta akavichanganya kwa pamoja huku
akiongea maneno fulani hivi kwa taratibu sana. Mwanzoni hata wale vijana
hawakuyasikia ila baadae kidogo yalipita vizuri kwenye ngoma za masikio yao.
“Mzilli... Mzilli... Cha cha
mziliii”
“Uwaano... Uwano kazi mziliiii”
“Uuutuu mziilli… Cha chaa”
“Uwaano... Uwano kazi mziliiii”
“Uuutuu mziilli… Cha chaa”
Alizidi kutamka maneno yale huku
akiwa anachanganya vile vitu kwa dakika hivi. Huku akiwa anaendelea
kuchanganya, hali ya hewa ilianza kubadiika. Wingu jeusi lilitanda juu ya anga,
mungurumo wa radi ulipiga, ulifanya vijana waliokuwa wakimsaidia Mzanzu Wazanzu
kuogopa sana.
Yeye akiendelea na kazi yake, mara
alinyamaza ghafla.
“Piteni hapa.” Kwa sauti ya kutisha iliyojaa utetemesho, mganga aliwaita wale vijana na kuanza kuwapa ule mchanganyiko. Wote waliokuwepo pale hali yao ilibadilika, wakaanza kuona vituko vya kichawi sasa mbele ya mboni zao.

Mzanzu Wazanzu aliagiza aletewe
kondoo yule halafu akanena,
"Kazi imeisha. Mimi sitowatajia nani anayesumbua kijiji chenu, ila mtamuona wenyewe. Kitu kimoja tu! Msishangae. Mkishaangaa tu! Hata mmoja wenu, litakalowakuta tusilaumiane nadhani tumeelewana vijana". Kwa sauti ya kuonesha msisitizo.

Haraka Mzanzu alipitisha kisu
shingoni kwa yule kondoo, damu zilimwagika na umwagikaji ule ulifanya sehemu
ile ibadilike. Vijana wakajikuta wapo katikati ya mkutano wa Wachawi
ukiongonzwa na Mzee Shabani.
Mandhari ya pale yalitisha sana. Maneno makali na ya Mzee Shabani yaliwatisha sana. Vijana waliona kama vile wanaonekana na Wachawi hao, la hasha hata punje ya taswira zao hazikuweza kuonekana mbele ya macho yao.

Huku wakiongonzwa na Mzanzu Wazanzu,
vijana walizidi kuoneshwa ukatili na unyama wa Mzee Shabani, kiongozi wa
Wachawi. Watu walipotea, ilizidi kuwatisha vijana hao na kuwaongezea machungu
ndani yao. Mzanzu aliwaonesha kila kitu.
Hatimaye Mzanzu Wanzanzu, kiboko ya
Wachawi, aliwaambia sasa kazi imekwisha na yeye hatoweza kulala pale kwa hali
ilivyo. Ila wale vijana ndio watawapa majibu viongozi na Wanakijiji wengine juu
ya kinachoikumba Tangeni. Walikubali na kila moja alirudi kwao huku wakiwa
hawamini walichokiona. Ila mganga Mzazu, hakuondoka hivihivi, aliwaachia dawa
vijana wale.
Asubuhi na mapema, la mgambo lililia
na kama unavyojua la mgambo likilia huwa lina jambo athirani. Hivyo jioni
waliitisha mkutano wakijiji na Wanakijiji wote walidhuria kwa wingi tofauti na
mikutano mingine inayotokea ndani ya kijiji cha Tangeni.
Ajenda kila mtu alifahamu, nini
tofauti na kawaida kabisa. Mara nyingi Mzee Shabani huwa ni mhudhuriaji mzuri
wa Mikutano, ila siku hiyo hakufika na watu walibaini kuwa hakufika kwenye eneo
lile. Japo haikushangaza, na kwa wengine waliamini tu hatakuwa labda tangazo
halijamfikia kutokana mkutano wenyewe kuitishwa ghafla, na kibaya zaidi nyumba
yake ilijitenga kivyake.
Mkutano ulifunguliwa mapema kabisa.
Mwenyekiti wa kijiji aliongea kwakina mchakato uliofanyika juu ya jambo lile.
Kila mmoja alielewa vizuri tu! Kutokana na mganga Mzanzu alivyowachia maagizo,
vijana wale ilibidi awape fursa ya kuongea iliwaweze kubaini nini walichokuwa
nacho vijana hao.
Siri, miongoni mwa vijana hao ndio
alipewa jukumu la kunzungumza kwaniaba ya vijana wale kumi na wawili.
Alinyanyuka na kuanza kuzungumza mambo waliyoyaona mwanzo hadi mwisho. Sasa
ikafika muda wakumtaja mhusika kuwa ni Mzee Shabani na wenzake. Siri alikuwa
kama amepigwa na ububu, ghafla hali yake ilibadilika, jasho lilimtoka kwa hali
ya juu kitendo kilichowafanya wanakijiji waogope sana, macho Siri aliyatumbua.
Hali yake ilibadilika sana, harakaharaka vijana walimbeba Siri.
Hata hawakufika mbali, Siri alipoteza maisha mikononi mwao. Kikao kiliahirishwa, na sasa watu wakajiandaa kufanya mipango ya mazishi. Kifo cha Siri kiliwatatanisha sana, kuogopesha miongoni mwa vijana wale.

Hali ilikuwa mbaya sana ndani ya
kijiji. Maziko ya Siri yalifanyika huku ikifatiwa na vifo vya wale vijana.
Wengine walikuwa miongoni waliteuliwa moja moja walipoteza maisha. Hali iitisha
zaidi ndani ya kijiji cha Tangeni.
Ni mmoja tu! Ndiye aliyebaki. Ndio
aliweza kuwaambia kinachowamaliza. Watu hawakuamini kuwa unyama wote unaotokea
ndani ya kijiji chao ni Mzee Shabani. Ndipo hapo baadhi ya vijana walikusanyika
wakiwa na majembe, wengine mapanga kwa hasira na chuki iliyosababishwa na
vitendo vya unyama wa Mzee huyo.
Vijana walizidi kupiga mayowe,
lakini hakuna mtu aliyejibu si Mzee Shabani wala mwanae Mwajabu, hata mkewe.
Ndani kulikuwa kimya tu.
_______________
Urembo wa Mwajabu Bint Shabani
ulikuwa tishio. Kila mtu alivutiwa nao. Umbo lake la wastani, macho yakulegea,
tabasamu lake, rangi nzuri ya maji ya kunde, ni vitu adimu sana. Wasichana
wengi hawana tofauti na Mwajabu. Tangia nimjue ndani ya kijiji chetu cha
Sitakishari, imeniletea shida ndani ya mtima wangu. Jack mimi, tatizo la moyo
acheni tu!
Sikujua nilizoeana naye vipi, ila
nilijikuta tumekuwa marafiki ndani ya muda mfupi tu. Japo ulikuwa ni urafiki wa
kawaida, ila nilikuwa naamini ipo siku utazaa matunda, na Mwajabu bint Shabani
atakuwa wangu siku moja. Sikuwa na mzaha hata kidogo, nilichohitaji siku moja
nikuwa Baba na yeye Mama wa watoto wetu.
Mazoea kati yangu na Mwajabu,
yaliongezeka siku hadi siku mpaka kuna baadhi ya watu zangu wa karibu walianza
kuhisi uenda kunakitu kinaendelea baina yangu na binti huyo. Vijiutani utani
vilikuwa haviishi, wengine mpaka waridiliki kuniita Baba Mwajabu. Ila mimi
niliona sawa tu, wananivimbisha kichwa. Kwa jinsi ya uzuri alionao Mwajabu,
kila mvulana ndani ya kijiji chetu, tangia ahamie pale, hakuna mtu aliyetaka
kucheza mbali. Kila mtu alikaba nafasi yake, ila mimi nilionekana nikojuu zaidi
ya vijana wenzangu wengine.
Namna mambo yalivyozidi kwenda, ndio
ukaribu ulizidi. Nakumbuka jana nilikuwa na Mwajabu kisimani tukiongea mambo
mawili matatu, dah! Kuna jambo aliniambia lilinishitua sana.
Kwajinsi ambavyo Mwajabu alivyokuwa akiniambia, nilizidi kuogopa. Niliogopa sana na moyo wangu ulikuwa kama umepigwa msumali ndani yake, na sasa Mwajabu maneno yake kwangu yalikuwa kama kuuchomoa au kuchoma zaidi moyo wangu. Namna alivyokuwa akiendelea kunena, alizidi kiniumiza. Kadiri alivyokuwa akiyatamka ndani ya kinywa chake hali yangu ilikuwa ikibadilika kwa muda mfupi tu.

Kwa jinsi moyo wangu ulivyozama
kwake, sikupenda hata kidogo maneno yale yalivyokuwa yakipenya ndani ya masikio
yangu yote mawili. Yalichoma choma ngome zangu za masikio na kuipoteza kabisa
furaha yangu. Si mimi tu! Niliyekuwa nikuumia na maneno yale, la hasha! Kwa
muonekano wake Mwajabu uliashiria kuwa maneno yale yalimchoma ijapokuwa yeye
ndio alikuwa akiyatoa kwenye kinywa chake
"Sikia Jack. Moyo wangu haupo,
hii wazi haupo kabisa na jambo ambalo Mzee analitaka. Hawezi kunichagulia mtu
wa kuishi naye mimi. Sijambo nzuri kabisa. Jack moyo wangu haupo kwake kabisa,
labda nikwambie ukweli tu. Mapenzi si yakulazimishana, ni tendo la kuridhiana
baina ya pande mbili. Naomba unisikilize Jack, huo ndio ukweli. Sipo
tayari." Aliongea Mwajabu namna alivyokuwa akiyanena maneno yale kwa hisia
kali kabisa yalizidi kunichanganya nisijue cha kufanya kabisa. Nilihisi kama
naota kumbe ndio ukweli.
Nilitafakari kwa kina jambo lile
bichi kabisa ndani ya kichwa changu. Ni jana tu ndio Mwajabu aliniambia kule
kisimani tulipokutana tukizungumza na mara nyingi sehemu hiyo ndio huwa
tunapataga fursa ya kuonana tofauti na sehemu nyingine ndani ya kijiji chetu.
Kwa mara ya kwanza ndipo nilipoanzisha mazoea na mdada yule na tangia hapo moyo
wangu ulipodondoka ndani ya penzi lake bila mimi kujua kuwa ndio nishapenda,
uwiiiii!
Nilimfahamu vyema Mzee wake kuwa ni
mkali si masihara, kama pilipili. hana utani hata kidogo. Baadhi ya vijana
wenzangu pale kijijini walinipenyezea balaa wanalokutana nalo pindi
wanapojaribu kusogea sogea maeneo ya Nyumbani kwake, si unajua tena vijana
wakijijini haswa kijiji chetu wakishaona mtoto mzuri katka kijumba fulani,
misele hahiishi .Hivyo suala lile lilikuwa gumu, nitamshawishi vipi nilijiuliza
hata majibu nilikosa mmmmh!
Riwaya hii ni endelevu ina sehemu 5 tutawaletea,......... endelea kufuatilia ili utate kujifunza
RIWAYA:
MTOTO WA MCHAWI WA KIJIJI
MWANDISHI: YONA FUNDI
MAWASILIANO: 0675278759
MWANDISHI: YONA FUNDI
MAWASILIANO: 0675278759
Post a Comment