Saudi Arabia
imejibu tangazo la Iran kwamba raia wake hawataruhusiwa kwenda kuhiji
Makka mwaka huu,kwa madai ya kwamba mamlaka ya Saudia imetengeneza
vikwazo kwa mahujaji wa Iran kushiriki Hijja hiyo.
Hata hivyo
Waziri wa Mambo ya nje wa Saudia Adel al-Jubeir amesema kuwa waumini hao
wa Kiislam kutoka nchini Iran,wanahitaji kupewa idhini pia ya kufanya
maandamano wakiwa nchiniSaudia jambo ambalo halikubaliki.
Iran inalaumu maafisa wa Saudia kwa vifo vya mamia ya mahujaji wake vilivyotokea mwakajana walipokwenda kuhiji.
Professor
Mohammad Marandi kutoka chuo kikuu cha Tehran,anasema wa hoja ya Iran,
ni kutaka kujiridhisha kama Mahujaji wake watakuwa salama katika Hijja
ya mwaka huu
"Raia wa Iran hawana namna. Maoni ya Wairan ni ya
hasira na jazba dhidi ya familia ya Kisaudia. Saudia imewakatalia Wairan
matumizi ya Kamera,ambazo ndizo zilizotumika kuonyesha picha za maelfu
ya watu waliokufa katika Hijja ya mwaka jana wakiwemo raia wa Iran. Na
kwa kuwa Saudia haikulezea mazingira halisi ya vifo hivyo na baadaye
ikaomba msamaha,Wairan wanaona bado mazingira hayajawa salama kwao kwa
ajili ya Hijja ya mwaka''.
Professor Marandi amesema vurugu zilizosababisha vifo katika Hijja mwaka jana hazikudhibitiwa vyema na serikali ya Saudia
"Saudia
ilionyesha bayana kutoheshimu mahujaji,familia zao na kwa miili ya
waliokufa, jambo ambalo kwa Wairan halikubaliki. Hivyo Wairan wanataka
kujua ni maboresho gani yatafanyika mwaka huu ili waweze kuwa salama
zaidi,lakini Saudia hawataki kuweka wazi kwamba ni mabadiliko gani
yaliyofanyika,na wakati huo huo viongozi wa dini nchini Saudia wanaamini
kuwa Wairan si waumini kamili wa dini ya kiislamu''.
Post a Comment