Leo ikiwa mei 27 Kulikuwa na mchezo mmoja wa robo fainali katika ligi ya kombe la mbuzi vijana cup mchezo uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Muungano wilayani Liwale ambapo kuliwakutanisha timu ya Sido fc Vs Mnala fc.
Mchezo wa leo ulikuwa mkali na uliovatia mashabiki wengi sana waishio Liwale mjini na viunga vyake,katika kipindi cha kwanza namo dakika ya 20 Hamanzi Hamanzi aliiandikia Mnalani fc goli la kwanza goli lililodumu mpaka mapumziko ya dakika 45.
Pindi cha pili dakika ya 47 Omari Issa aliongeza goli la pili baada ya golikipa wa Sido fc kuuzalau mpira ulipigwa mbali alipojaribu kuupiga aliukosa na kushindwa kugeuka haraka ndipo Omari Issa alipata mwanya kwa kuukimbilia mpira huo na kuuweka nyavuni kwa hulaini huku akiwaacha baadhi ya wachezaji wa Sido fc wakiangua kilio.
Dakika ya 48 Haikosi Mpwate aliiandikia Sido fc goli la kwanza baada ya kupata basi safi na dakika ya 54 Ismaili Maleta aliipatia Sido fc goli la pili lakini magoli hayo hayakudumu richa ya sido fc kuangaika walishangaa dakika ya 56 Imamu Ahmadi aliiongezea Mnalani goli la tatu magoli yaliodumu mapaka dakika 90 za mchezo zinamalizika matokeo yalikuwa Sido fc 2-3 Mnalani fc.
Kocha wa timu ya Sido fc Mohamedi Farijala alisema amekubali kichapo cha goli 3 kwa 2 ndio matokeo ya mchezo ila anajipanga kwa ligi ijayo nae kocha wa Mnalani fc Abasi Malunga alisema baada ya ushindi wa leo ana imani ya kushinda kombe japo amewahofia timu pinzani ya Wakaanga Sumu lakini amejiipata moyo atashinda kwani wachezaji wake wanauzoefu wa kutosha kwa sasa.
Kesho mei 28 kutakuwa na mchezo kati ya Vijuso fc Vs Kombaini fc mchezo unaosubiliwa kwa hamu sana na mashabiki wa kila timu mchezo huu utatimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano-Liwale Mjini
Kesho mei 28 kutakuwa na mchezo kati ya Vijuso fc Vs Kombaini fc mchezo unaosubiliwa kwa hamu sana na mashabiki wa kila timu mchezo huu utatimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano-Liwale Mjini




Post a Comment