Serikali ya Tanzania imeagiza sukari ilikukabiliana na upungufu wa sukari uliopo nchini.
Rais wa
Tanzania Joseph Pombe Magufuli amesema badala ya kuwapa wafanyabiashara
leseni ya kuagiza sukari kutoka ng'ambo serikali yenyewe ndio itaagiza
sukari hiyo moja kwa moja.
Kauli
hiyo inawadia baada ya mabohari zaidi kugunduliwa kote nchini yakiwa
yamejaa sukari iliyoagizwa kutoka nje na ile iliyonunuliwa kwa wingi
kutoka kwenye kampuni za kusaga sukari za humohumo Tanzania.
''Kuna
mmoja ambaye amepatikana Arusha amehodhi zaidi ya tani elfu tano ya
sukari naye mwengine huko Kilombero amenunua sukari yote kutoka kwa
kampuni za humu humu nchini na akaficha.''
''Lakini
hili ni swala la sasa tu, katika siku zijazo sukari itapatikana kwa
wingi hapa Tanzania.Serikali imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa
hawa waliofilisi watanzania leseni ya kuingiza tena sukari.
''Serikali
imeagiza na itauza sukari hiyo kwa bei ya chini,,,, hiyo ndio lengo la
serikali '' alisema rais Magufuli huku mawananchi wakimshangilia.
Image caption''Katika
siku zijazo sukari itapatikana kwa wingi hapa Tanzania.Serikali
imekwisha agiza sukari lakini hatutawapa hawa waliofilisi watanzania
leseni ya kuingiza tena sukari.''
Sukari hiyo ambayo huwa ni ya bei ya chini hubadilishwa na kisha kuvikwa
magunia ya makampuni ya Kitanzania yanayosaga sukari na kisha kuuzwa
rejareja.
Tumbua tumbua ya rais Magufuli imesadifiana na tangazo la Halmashauri ya
ushuru ya Tanzania TRA kuwa imeanza kugawa sukari iliyoingizwa nchini
kinyume cha sheria na kufichwa katika mabohari kote nchini.
TRA ilichukua hatua hiyo baada ya mwekezaji wa kibinafsi mkoani Lindi
kupatikana na zaidi ya mifuko elfu tano za sukari kutoka nga'mbo.
Yamkini sukari hiyo hubadilishwa kwenye mifuko yenye nembo ya kampuni za
kusaga sukari za Tanzania na kisha kuuzwa kwa bei maradufu.
Post a Comment