Abilah Kimbalala kocha wa timu ya Nangando fc akitoa maelezo kwa wachezaji wake angalau wapate goli za kufuati machozi lakini juhudi zake ziligomba mwamba hii leo
Ikiwa may 13 katika ligi ya mbuzi vijana cup inayoendelea hapa wilayani Liwale hatua ya makundi leo kulikuwa na mchezo katika kundi A kulikuwa na mechi kati ya Mnalani Vs Nangando FC mchezo uliotimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano.
Namo mara baada ya kuanza mpira dakika ya 5 Abedi Iluline aliiandikia timu ya Mnalani goli la kwanza na dakika ya 10 Imamu Ahmadi aliandikia Mnalani goli la pili magoli hayo yalidumu mpaka mapumziko.
Katika kipindi cha pili Abedi Iluline aliapachika Mnalani fc goli la tatu katika dakika ya 60 na goli la nne la Mnalani fc lilipachikwa na Imamu Ahmadi katika dakika ya 70 na kuifanya Mnalani fc kuwa timu ya kwanza kufuvu katika hatua ya makundi.
Abilah Kimbalala kocha wa timu ya Nangando fc alisema mchezo wa leo ulikuwa mzuri lakini wachazaji wake wamekosa pumzi lakini alijipa matumaini ya kushinda kwa mechi ijayo nae kocha wa Mnalani fc Kasimu Malunga alisema mchezo wa leo ulikuwa mzuri na amejipa matumaini hatua ya 8 bora atafanya vizuri zaidi kwakuwa yeye anambinu nyingi za ushindi wa kimichezo.
Post a Comment