Meli kubwa ya Marekani Adonia, ikiwa na abiria mia saba ndani yake ikielekea Cuba.
Meli ya kifahari ya
Marekani imeanza safari yake kuelekea Cuba ikitokea nchini Marekani kwa
mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
Meli
hiyo iitwayo Adonia, imebeba abiria wapatao mia saba,imeng'oa nanga
kutoka katika bandari ya Miami na inatarajiwa kufika tamati ya safari
yake Jumatatu ijayo.Cuba na Marekani zimerejesha uhusiano baina yao wa kidplomasia mwaka wa jana, ingawaje vita baridi iliyokuwa baina ya nchi hizo ilisababisha hali kibiashara kati yao kuwa ya kusua sua na bado hali si shwari mpaka sasa.
Post a Comment