Watoto Keith, Ali, Penelope, Tiffany na Beatrix Mama mmoja raia wa Australia ametoa picha za mapacha watano aliowazaa mwezi Januari.
Kim Tucci wa miaka 26 alichukua dadika mbili tu kujifungua wanawe hao, wasichana wanne na mvulana mmoja.
Wote walitungwa kawaida, hakutumia matibabu yeyote ya uzazi.
Bi Tucci alipata umaarufu sana wakati alipoweka taarifa za mimba yake katika ukurasa wake wa Facebook.Kampuni ya kunasa picha ya Erin Elizabeth imesaidia sana kunadi safari ya Bi Tucci wakati wa uja uzito wake.
Hata hivyo aliamua kubeba mimba yake hadi mwisho.
Bi Tucci na mumewe bwana Vaughn wana watoto watatu mvulana na wasichana wawili.Wameanza kuchangisha pesa ili kununua gari kubwa ambalo litaweza kukimu familia hiyo kubwa.
Post a Comment