JESHI la askari wa miguu wa nchi kavu kutoka Tanzania, limeonesha zoezi
maalumu la kuteka na kudhibiti adui kwa kwa wakuu wa Kamandi za Nchi
Kavu kutoka nchi zaidi ya 36.
Zoezi hilo lilifanyika eneo la Mafunzo ya Kijeshi wilayani Monduli mkoa wa Arusha, ambako wakuu hao wa majeshi ya nchi kavu walitembelea kujionea jinsi Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linavyoweza kukabiliana na maadui.
Akizungumza na wanahabari juzi, Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu, Meja Jenerali, James Mwakibolwa alisema zoezi hilo ni kwa ajili ya kuwaonesha wakuu wa kamandi za majeshi ya nchi kavu jinsi gani jeshi la nchi kavu la Tanzania linavyoweza kukabiliana na maadui.
Alisema pia limeonesha jinsi ya kufanya mashambulizi, ikiwemo kupiga mizinga, mapambano ya kuangamiza vikundi vingine ambavyo vinamweka adui chini, ikiwemo kupambana na adui kwa mapigo na kuwa na vifaa vya kisasa.
Pia alisema zoezi hilo ni kuonesha uzalendo na kujituma kufanya kazi katika kuimarisha ulinzi wa nchi. Wakati zoezi likiendelea, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani, Mark Milley aliinuka kwenye kiti na kuanza kushangilia.
Mnadhimu huyo kutoka Marekani, Milley alieleza kufurahishwa na mashambulizi hayo huku akisifu jeshi la nchi Kavu la Tanzania kuwa ni zuri.
Wakuu hao wa kamandi za nchi kavu wapo nchini kwenye mkutano unaolenga kuendeleza ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayolikabili Afrika katika ulinzi.

Post a Comment