0


Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) mkoani Mtwara  limelazimika  kusimamisha Magari na Pikipi kuwashusha watu ili wajumuike katika kufanya usafi unaofanyika kila mwisho wa mwezi baada ya  zoezi hilo kuonekana kusuasua na kufanywa na wananchi wachache zikiwemo taasisi za serikali.

Akiongoza zoezi hilo la kufanya usafi Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego amesifu taasisi zilizojitokeza yakiwemo majeshi ambayo yamesaidia watu wengi kujitokeza na kufanya usafi.

Wakizungumzia usafi huo wa mazingira baadhi ya wananchi wamesifu zoezi hilo na kutaka wananchi kujitokeza kila mwisho wa mwezi wingi ili kufanya usafi ambao ni muhimu kwa afya.

Zoezi la kufanya usafi katika mkoa wa mtwara limekuwa likihamasishwa sana na vyombo vya habari vilivyopo mkoani humo,na ikumbukwe,  lilizinduliwa na Mh Rais John Pombe Magufuli Disemba tisa mwaka jana.

Post a Comment

 
Top