Akizungumza na ITV Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu Kamshina Msaidizi wa polisi Onesimo Lyanga amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na kukithiri kwa matukio ya ukataji mapanga katika mkoa huo.
Aidha katika tukio jingine Kamanda Lyanga amesema jeshi hilo limefanikiwa kupata bunduki moja ya kivita aina ya SMG ikiwa na risasi 20 ambayo ilisalimishwa na watu wasiofahamika nyumbani kwa mwenyekiti wa kijiji cha Longalobogo wilayani itilima.
Kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa hao kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu kuendelea kutoa taarifa kwa jeshi hilo pale wanapoona kuna matukio ya uharifu ili mkoa uweze kuwa salama.
Nao baadhi ya wananchi wa mkoa huo wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada wanazofanya za kupambana na uharifu ambapo wameahidi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

Post a Comment