Ni moja ya barabara ya kuelekea katika ofisi ya chama cha bodaboda
Baadhi ya viongozi wa chama cha bodaboda kama m/kiti Bw.Rafii Likochelo na wajumbe wakisimamia ujenzi wa ofisi ya chama cha bodaboda iliyopo katika kijiji cha Mungurumo karibu na ofisi za Idara Maji wilaya
Katika harakati za kujikwamua na umasikini kwa vijana chama
cha waendesha tax,bajaji na pikipiki (bodaboda) cha wilayani Liwale mkoani
Lindi kilianza rasmi mwaka 2014 kikiwa na wanachama 65 hadi sasa mwaka 2016
kina jumla ya wanachama 300.
Chama cha hiki kwa kushiriana viongozi wa chama na wanachama
kimeweza kukopesha pikipiki 65 na vifaa
mbalimbali vya ujenzi kwa wanachama wake toka mwaka 2014 hadi februaru 2016.
Kila kazi mara nyingi au hulenga na fanyikio,katika chama
hiki cha bodaboda kimeweza kufanyikiwa kwa kuweza kupata mambo mbalimbali kwa
ushirikiano na viongozi mbalimbali wa kisherikali na viongozi wa vyama vya
ushirika na wafanyabiashara walioko ndani ya wilya ya Liwale.
Baadhi ya mafanyiko ya chama cha bodaboda ni
Kimeweza kuongeza matawi ya wanachama wa bodaboda kutoka
matawi 4 mpaka sasa kuwa na matawi 7 baadhi ya matawi hayo yapo vijijini kama
vile Likombola na Mpengele.
Kumiliki uwanja na
kujenga ofisi ya chama kwa ushirikiano na viongozi mbalimbali wa serikalini na
wadau wengine waliowezesha chama kupata uwanja na kujenga ofisi.
Kupata mikopo kutoka serikalini ya asilimia 5 (5%) ya vijana.
Richa ya kuwa na ma kufanyikiwa zipo changamoto wanazokumbana nazo kama vile
Uwezeshaji mdogo wa kifedha katika chama cha bodaboda hivyo
hushindwa kuendesha shughuli mbalimbali za kichama kwa wakati hivyo hutegemea
michango yao lakini haimalizi mahitaji
Usumbufu wa askari barabarani baada ya viongozi walibainisha
kuwepo kwa usumbufu kwa baadhi ya askari polisi kuwasumbua waendesha bodaboda.
Kunyang`anywa kwa pikipiki,viongozi walibainisha toka chama
kianzishwe rasmi mwaka 2014 mpaka mwaka 2016 kumetokea na kuuawa kwa mwanachama
wao mmoja na kung`ang`anywa pikipiki 6.
Chama cha bodaboda kina ushirikiano mzuri kati ya chama na
viongozi mbalimbali wa serikalini ikiwemo na Mkuu wa wilaya ya Liwale mh.
Ephraim Mmbaga aliweza kuwaunganisha wanachama wa bodaboda baada ya chama hiko
kuingia kwenye mpasuko.
Mbali ya kuwaunganisha wanachama mkuu wa wilaya mh. Mmbaga
alikisaidia chama cha bodaboda mawazo chanya na kusaidia chama kupata mkopo wa pikipiki na uwanja wa ofisi na
ujenzi wa ofisi ya chama cha bodaboda.
Nae mbunge wa jimbo la Liwale, mh. Zuberi Kuchauka ameonesha
ushiriano wake kwa kuwaweza vijana hao kuwapatia fedha za mfukom wa jimbo kiasi
cha shilingi milioni 2.5 kwa ajiri ya kuendeleza ujenzi wa ofisi ya chama cha
bodaboda.
Wapo wafanyabiashara walionesha kushirikiano mkubwa na msaada
kwa vijana wa chama cha bodaboda kama
Amidu Wamo ambaye amewakopesha chama cha bodaboda pikipiki 42 na chama
hurejesha malipo kidogo kodogo na kwa awamu.
Baadhi ya wadau wengine wameweza kukisaidia chama cha
bodaboda kama chama cha ushirika umoja pamoja na mwenyekiti wa chama hiko Bw.
Hasani Mpako kwa kuweza kuchangia bati 20 pamoja na chama cha ushirika Umoja
kiliweza kuchangia pia bati 20 za ujenzi wa ofisi ya bodaboda na baadhi ya
viongozi wengine waliosaidia chama kwa namna moja pamoja na ofisi ya Maendeleo ya jamii Wilaya na seluu.
Post a Comment