0


Bosi wa timu ya Azam FC, Yusuph Bakhresa ameamua kumtoa bure Farid Mussa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Hispania.

Mwezi uliopita Farid alifanikiwa kwenda nchini Hispania kwenye timu ya Club Deportivo Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo kwa ajili ya kufanya majaribio na hatimaye alifaulu majaribio hayo na kusubiri uongozi wa timu zote mbili zikae mezani zikubaliane.

Yusuph Bakhresa alisema, “Wapo watu walikuwa wanaingilia kati dili hili na kutaka kufanya ujanja ujanja ili kutudhulumu lakini kama mmiliki wa Azam nimefanya mazungumzo na klabu ya Tennarife na tumekubaliana kumtoa bure mchezaji huyo na endapo klabu hiyo itamuuza ndipo watatupa pesa kwa makubaliano yatakayokuwa kwenye mkataba wake.”

Farid ataondoka nchini kuelekea nchini Hispania kujiunga na timu yake hiyo mpya Tenerife baada ya fainali ya mechi ya FA itakayofanyika siku ya Jumatano kwenye uwanja wa taifa.

Post a Comment

 
Top