wamiliki wa mashamba ya kuku kutoka mataifa mbalimbali wameonesha kuvutiwa na ndege hao kutokana na kutolazimika kuwanyonyoa baada ya kuchinjwa!
Wanasayansi waliozalisha kuku hao wamesema kuwa, jamii ya kuku wa aina hii ni salama kwa afya ya mlaji.
Isitoshe, wanakua haraka na nyama yao ina kiwango kidogo cha mafuta,tofauti na jamii nyingine za kuku.
Profesa Avigdor Cahaner,ambaye ni mkuu wa mradi huo katika chuo kikuu cha kilimo mjini Rehvot, Israel, alimsema kuwa manufaa ya kuku hao ni makubwa kiuchumi na kijamii na kusisitiza kuwa hata kwa mfugaji gharama za kuwahudumia zitapungua kwani hakutakuwa na haja ya kuwawekea viyoyozi kwenye nchi zenye joto.
Post a Comment