Droo ya Nusu
Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imefanyika
jana huku timu za Coastal Union na Mwadui FC zikipata nafasi ya kucheza
nyumbani.
Katika droo hiyo iliyochezeshwa na mchezaji mstaafu wa
timu ya timu ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), Esther Chaburuma,
imewashuhudia vigogo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, Azam FC na Young
Africans wakipata nafasi ya kucheza michezo hiyo katika viwanja vya
ugenini.
Mwadui FC watakua wenyeji wa Azam FC katika mchezo
unaotarajiwa kucheza Aprili 24, 2016 mjini Shinyanga, huku wagosi wa
Kaya Coastal Union wakicheza dhidi ya Young Africans katika uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga siku hiyo hiyo.
Washindi wa michezo hiyo ya
Nusu Fainali, watakutana fainali ya kombe hilo itakayofanyika mwezi
Mei, ambapo Bingwa wake ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe
la Shirikisho barani Afrika (CAF).
Na Ligi Kuu ya Tanzania bara
inatarajiwa kuendelea tena leo Jumatano, kwa michezo miwili katika
viwanja vya Manungu Turiani mkoani Morogoro na uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam.
Young Africans wanaoshika nafasi ya pili kwenye
msimamo wa ligi, watakua wenyeji wa Mwadui FC inayokamata nafasi ya sita
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wakata miwa wa
Turiani, Mtibwa Sugar walio katika nafsi ya nne ya msimamo wa ligi kuu
watawakaribisha Azam FC walio juu yao nafasi ya tatu, mchezo
utakaochezwa katika uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro.
Post a Comment