Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Rais wa
Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
(Mechanism for International Criminal Tribunals-(MICT) inayojengwa
katika eneo la Lakilaki jijini Arusha, Mhe. Theodor Meron. Rais huyo
alifika Wizarani kwa ajili ya kujitambulisha kwa Mhe. Waziri, kumweleza
maendeleo ya ujenzi wa Mahakama hiyo pamoja na kuishukuru Serikali ya
Tanzania kwa ushirikiano na mchango mkubwa inaotoa katika kufanikisha
ujenzi huo. Pia aliipongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika
kusimamia utawala wa sheria na haki.
Picha na Reginald Philip
Mhe. Mahiga na Mhe. Meron
Mhe. Mahiga akiagana na Mhe. Meron
...........Mkutano wa Waziri na Mwendesha Mashitaka wa MICT
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mwendesha
Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya
Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International Criminal Tribunals-
(MICT), Mhe. Dkt.Serge Bremmertz. Katika mazungumzo yao Mwendesha
Mashtaka huyo aliipongeza Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kuridhia
taasisi za Umoja wa Mataifa zinazosimamia sheria kujengwa nchini na
kuielezea Arusha kama makao makuu ya kimataifa ya haki kwa Ukanda wa
Afrika. Pia aliahidi ushirikiano hususan katika kuwajengea uwezo
wataalam wa masuala ya sheria za kimataifa hapa nchini.
Sehemeu ya Wajumbe waliofuatana na Mwendesha Mashtaka wa MICT.
Mazungumzo yakiendelea. Kushoto kwa Mhe. Mahiga ni Bw. Elisha Suku,
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Mhe. Dkt. Mahiga akiagana na Mwendesha Mashtaka wa MICT, Dkt. Brem
Post a Comment