Afisa Mkuu anayeushughulikia mgogoro wa wakimbizi nchini Ujerumani ametoa wito kwa serikali binafsi za majimbo ya nchi hiyo kuongeza maradufu idadi ya waomba hifadhi wanaofukuzwa nchini humo ambao maombi yao yamekataliwa. Peter Altmaier ameyaambia magazeti ya kampuni ya habari ya Funke kuwa katika mwaka wa 2015, waomba hifadhi 37,220 walirejea nchini mwao kwa hiari, wakati waomba hifadhi 22,200 waliokataliwa maombi yao wakifukuzwa. Altmaier ambaye ni mkuu wa baraza la mawaziri la Kanseka Angela Merkel na amechaguliwa kuongoza juhudi za kuutatua mgogoro wa wakimbizi amesema itakuwa jambo la msingi kwa serikali za majimbo ya Ujerumani kuongeza maradufu takwimu hizo katika mwaka huu wa 2016. Serikali kuu ya Ujerumani imekuwa kwa muda sasa ikisisitiza kuwa waomba hifadhi wanaokataliwa maombi yao wanapaswa kurejeshwa nchini mwao haraka.
Waomba hifadhi wanaokataliwa na Ujerumani wafukuzwe haraka

Post a Comment