Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta amezichoma pembe za ndovu katika juhudi za kuonyesha taifa
lake kuhusu umuhimu wa kuwahifadhi ndovu.
Zaidi ya tani 100 za
pembe za ndovu zilikusanywa katika mbuga ya wanyama ya Nairobi ambapo
zinatarajiwa kuchomeka kwa siku kadhaa.Pembe hizo zinawakilisha karibia pembe zote zilizopatikana na serikali zikidaiwa kutoka kwa takriban ndovu 6,700.
Hatahivyo wengine wametofautiana na hatua hiyo ya Kenya wakisema inaweza kuongeza visa zaidi vya uwindaji haramu.
Kabla ya kuwasha moto huo,Bw Kenyatta alisema: Wingi wa Pembe hizi ndio unaotupatia shinikizo zaidi kukabiliana na visa vya uwindaji haramu.
''Hakuna na narudia hakuna mtu aliye na sababu ya kushiriki katika biashara ya pembe za ndovu''.
Post a Comment