Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania
chini ya umri 17 leo watashuka dimbani kucheza mchezo wa kujipima
nguvu dhidi ya timu ya Misri Mafarao.
Mchezo huo utachezwa kwenye
uwanja wa Azam Complex, ni mchezo wa marudiano ambapo mchezo wa kwanza
ulichezwa jumamosi iliyopita katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaa.
Mchezo
utachezwa saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati,
Katika mchezo wa kwanza Serengeti boy walishinda kwa ushindi wa mabao
2-1.
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maaandalizi kwa timu zote
Tanzania (U17) na Misri (U17) zinazojiandaa na michezo ya kuwania kufuzu
kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana mwaka 2017 zitakazofanyika
nchini Madagascar.
Post a Comment