Somalia inatazamia kuwazuia vijana ambao hufanya safari hatari kwenda Ulaya
Somalia imewaambia
raia wake kuwa hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchini Sudan, ambacho ni
kituo maarufu kwa wahamiaji wanaosafiri kwenda Ulaya kinyume na sheria.
Afisa
mkuu wa uhamiaji Abdullahi Gafow, alisema kuwa wasomali ambao
wataruhusiwa kusafiri kwenda Sudan ni wale wanaohusika na masuala ya
kidiplomasia.Bwana Gafow alisema kuwa anatazamia kuwazuia vijana wa kisomali ambao hufanya safari hatari kwenda Ulaya.
Mamia ya wahamiaji wengi wao rais wa Somalia, wanaripotiwa kufa maji mapema wiki hii wakati mashua yao ilizama katika bahari ya Mediterranean.
Post a Comment