Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amepenyoka kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.
Zuma alipata kura kutoka kwa wabunge 233 wanaomuunga mkono dhidi ya 143 za wabunge ambao hawakuwa na imani naye.
Awali
naibu spika alikuwa amewataka wabunge wapaze sauti hadharani kuhusu
iwapo alikuwa anaunga mkono kura ya kutokuwa na imani au la.
Hata hivyo upinzani ulishinikiza kura hiyo iendeshwe kwa njia halisi sawa na kura zingine.
Wachanganuzi
wa maswala ya kisiasa nchini Afrika kusini walikuwa wanatarajia matokeo
hayo kutokana na idadi kubwa ya wabunge wa chama tawala cha ANC.
Bunge la
Afrika Kusini liliamua kusikiza na kujadili hoja ya kumng'oa rais Jacob
Zuma kufuatia shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani.
Spika wa
bunge la Afrika Kusini bi Baleka Mbete, alikubali hoja hiyo ijadiliwe
kufuatia mahakama ya juu ya Afrika Kusini kumpata rais Zuma na hatia ya
matumizi mabaya ya madaraka yake.
Chama cha
Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema
kilienda mahakamani kikitaka rais Zuma ashurutishwe kulipa fedha
zilizotumika kinyume cha sheria kufanya ukarabati katika makazi yake ya
Nkandla.
Upinzani
uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka
2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba
alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.
Post a Comment