Mwaandishi wetu
Mfuko
wa hifadhi ya jamii NSSF mkoani Lindi imewafikisha mahakamani waajiri watatu
wanaokabiliwa na kosa la kutolipa madeni ya jumla ya shilingi milion 116
Akizungumza
na waandishi wa habari Katika mkutano wa wadau uliyoketi kujadili changamoto za
mfuko huo meneja wa Nssf Mkoa wa Lindi Nuru Azizi amesema mfuko hauta wavumilia
wateja ambao wamekuwa wakikiuka utaratibu wa kulipa madeni yao kwa wakati na tutawafikisha waajiri wasio waminifu kwenye vyombo vyombo vya kisheria.
Amesema
kufuatia uhamasishaji uliyofanywa na mfuko huo mkoa wa lindi unazaidi ya
wananchama 3000 ambapo kati yao wapo wateja(waajiri) watatu ambao
wameshafikishwa kizimbani wakikabiliwa na madeni ya jumla ya shilingi milioni
116.
Afisa
shughuli mwandamizi Kabonwa Kandoro alisema mfuko una unatoa mafao mbalimbali
ikiwemo mafao ya muda mrefu ambayo ni uzeeni, ulemavu, urithi, mafao ya muda
mfupi ni matibabu, uzazi, kuumia kazini mazishi,
Akizungumza
kwa niaba ya waajiri Mohamedi Khamisi alisema licha ya huduma bora zilizopo
lakini bado zipo changamoto za upotevu na taarifa kitendo kinachopelekea
kucheleweshwa kwa huduma.
Khamisi
ameuomba mfuko kuhakikisha kuwa taarifa zinafika kwa wakati ili kupunguza
migongano na migogoro kati ya mfuko na waajiri.
Post a Comment