Kwa upande wa Azam FC walikuwa Shinyanga katika uwanja wa Mwadui FC kucheza mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup), Azam FC wapo katika uwanja ambao inaaminika ni mgumu kwa mgeni kupata matokeo hususani katika mchezo muhimu kama huu wa nusu fainali.
Mchezo ulianza kwa Azam FC kupata goli la kwanza dakika ya 3 kupitia kwa Hamisi Mcha, goli ambalo lilisawazishwa na Kabunda na kufanya dakika 90 zimalizike kwa sare ya goli 1-1, mambo yalibadilika baada ya kuanza kwa dakika 30 za nyongeza na Hamisi Mcha akapachika goli la pili kwa Azam FC lakini Jabir Aziz akaisawazishia Mwadui FC dakika moja kabla ya dakika 120 za mchezo kumalizika.
Hata hivyo mechi ililazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penati na Azam FC ikaibuka ushindi wa penati 5-3, mikwaju ya penati ilipigwa baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya goli 2-2. Azam FC sasa inasubiri mshindi kutoka katika mchezo uliyovunjika kati ya Yanga na Coastal Union.
Post a Comment