0

Mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Mangochie 

Geita. Muuguzi wa zahanati ya Kagu  wilaya ya Geita mkoani hapa, Elizabeth Misango (54) ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Japokuwa Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo la kikatili mkoani hapa, mashuhuda wanahusisha mauaji hayo na imani za kishirikina.

Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo, mkuu wa wilaya ya Geita Manzie Mangochie mauaji hayo yametokea jana usiku baada ya wanaume watatu kufika nyumbani kwa marehemu wakidai wana mgonjwa na Misango alipotoka kuwasikiliza shida yao, ndipo walipomvamia na kwa kutumia panga na kusababisha kifo cha muuguzi huyo.

Post a Comment

 
Top