Mmiliki wa klabu ya African Lyon itakayoshiriki ligi kuu ya soka
Tanzania 2016-17, Rahimu Zamunda amekanusha taarifa za kuuzwa kwa klabu
hiyo ambayo imekuwa katika harakati za kujiendesha kibiashara kama
ilivyo Azam FC.
Zamunda amekanusha taarifa hizo, kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwamba tajiri wa kiarabu Suleyman Alfahim amefikia makubaliano ya kuinunua klabu ya African Lyon.
Akifafanua juu ya taarifa hiyo Zamunda amesema ni kweli African Lyon imefanya mazungumzo na tajiri huyo kutoka nchini Dubai, lakini si kwa minajili ya kuuziwa klabu kama inavyoendelea kuzungumzwa tangu mwanzoni mwa juma hili.
Kiongozi huyo amesisitiza kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanapata kiongozi ambaye ana uzoefu na uwezo wa kuinyanyua klabu yao pamoja na soka la Tanzania ambalo linahitaji kujikwamua kutoka hapa lilipo.
African Sports imefanikiwa kurejea tena katika ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu ujao kufuatia kufanya vizuri kwenye kundi A la ligi daraja la kwanza huku ikivipiga kumbo vilabu vya Friends Rangers na Ashanti United.

Post a Comment