Shiza Ramadhani Kichuya
Mshambuliaji Shiza
Ramadhan Kichuya wa timu ya Mtibwa Sugar amechaguliwa kuwa mchezaji bora
wa mwezi Machi kwa Ligi Kuu Tanzania Kichuya alionyesha kiwango cha juu
katika mwezi huo uliokuwa na raundi nne, hivyo kuisaidia timu yake
kushinda mechi mbili kati ya tatu ilizocheza.
Katika mechi hizo
ambazo zote Kichuya alicheza, alifanikiwa kufunga mabao mawili kati ya
matano yaliyofungwa na timu yake. Alifunga dhidi ya Coastal Union kwa
ushindi wa mabao 3-0, na JKT Ruvu Stars ambapo Mtibwa Sugar ilishinda
mabao 2-1.Washindani wa karibu wa Kichuya walikuwa washambuliaji Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar, na Abdulrahman Mussa wa JKT Ruvu Stars ambao pia waling'ara kwa upande wa timu zao kwa mwezi huo.
Kichuya ambaye huu ni msimu wake wa pili kwenye Ligi Kuu, kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora kwa Machi atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo.
Post a Comment