0

Real-Madrid-legends

Jumamosi ya April 2, 2016 kulikuwa na mchezo mkubwa wa ligi ya Hispania kati ya Barcelona dhidi ya Real Madrid uliochezwa kwenye uwanja wa Capm Nou na kuishuhudia Madrid ikiituliza Barcelona kwa bao 2-1 na kumfanya kocha wa Madrid Zinedine Zidane kuifunga Barcelona kwa mara ya kwanza akiwa kama kocha.
Juma lililopita mtandao huu ulikuletea mfululizo wa mambo kadha wa kadha yakihusu mchezo wa El Clasico (Barcelona vs Real Madrid) lakini leo mambo ni tofauti.
Real Madrid ina rekodi nyingi sana kwenye soka la Hispania na Ulaya kwa ujumla, www.shaffihdauda.co.tz inakuletea mambo saba (7) ambayo pengine ulikuwa huyafahamu yote kuhusiana klabu ya Real Madrid.
Champions League La decima
Mara mwisho kutwaa taji hilo ilikuwa ni mwaka 2014 walipoifunga Atletico Madrid kwa bao 4-1 wakati wa dakika za nyongeza.
Miaka ambayo Madrid imechukua taji hilo na kutengeneza histonia ya miaka kumi (10): 1956, 1957, 1958, 1959, 1960,1966,1998, 2000, 2002, 2014.
AC Milan ni klabu ya pili ikiwa imetwaa taji hilo mara 7 wakati Barcelona wao wamelichukua mara 5 mara mwisho ikiwa ni msimu wa 2014-2015.
2. Real Madrid ndiyo klabu yenye mataji mengi la La Liga 
la liga
Imefanikiwa kutwaa jumla yaa mataji 32 ya kombe la La Liga, mara ya mwisho kutwaa kombe hilo ilikuwa ni mwaka 2012. Barcelona klabu ya pili ikiwa imetwaa kombe hilo mara 23 huku taji lao la hivi karibuni likiwa la msimu uliopita 2014/25.
3. Real Madrid imetwaa taji la Copa del Rey (kombe la Mfalme) mara 19
Copa del Rey
Barcelona imechukua ndoo hiyo mara 27, wakiwa bado wanashikilia ndoo hiyo waliyoitwaa msimu uliopita 2014/2015.
4. Real Madrid inashikilia rekodi ya UEFA ya ushindi mkubwa wa nyumbani kuwahi kutokea kwenye michuano ya Ulaya
Real Madrid Squad (1961-62)
Real Madrid Squad (1961-62)
Waliifunga klabu ya Odense BK kwa magoli 9-0 tarehe 25/10/1961hatua ya raundi ya kwanza mechi ya marudiano ya michuano ya  European Champion Clubs’ Cup kwasasa UEFA Champions League.
5. Real Madrid bado inashikilia rekodi ya UEFA ya ushindi mkubwa wa ugenini kuwahi kutokea kwenye michuano ya Ulaya
Real Madrid Squad 1969-70
Real Madrid Squad 1969-70
Real Madrid iliichapa Olympiakos Nicosia FC kwa jumla ya magoli 8-0 tarehe 24/09/1969 ikiwa ni michuano ya European Champion Clubs’ Cup raundi ya kwanza mchezo wa kwanza.
6. Real Madrid imewahi kupokea kipigo kikubwa kutoka kwa AC Milan 
1989 VS AC MILAN
Kikosi cha Madrid kilipoteza mchezo kwa kuchapwa bao 5-0 mara mbili kutoka kwa miamba ya soka la Italia tarehe 19/04/1984 kwenye michuano ya European Champion Clubs’ Cup hatua ya nusu fainali mchezo wa marudiano.
7. Real Madrid ilianzishwa mwaka 1902 huku jina lao la utani likiwa ni Los Merengues (The Meringues)
Real Madrid (
Real Madrid (1905-06)

Post a Comment

 
Top