David Kafulila
Ferinand Wambari,
Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora ametupilia mbali hoja za
mawakili wa Husna Mwilima, Mbunge wa Kigoma Kusini na serikali dhidi ya
David Kafulila ambapo waliwasilisha nyaraka za kurasa zaidi ya 300
kuomba kesi aliyoifungua Kafulila mahakamani hapo ifutwe.
Katika
hoja zilizowasilishwa na mawakili wa Mbunge Mwilima wamesema, baada ya
Kafulila kuwasilisha vielelezo na mashahidi watatu mahakamani hapo
hawaoni kesi ya kujibu .
Akifuta hoja hizo mahakamani Jaji Wambari amesema, Husna anapaswa kutoa ushahidi uliompa ushindi na kuagiza msimamizi wa uchaguzi huo kutoa ushahidi uliopelekea kumtangaze Husna Mwilima kama mshindi wajimbo hilo.
Akifuta hoja hizo mahakamani Jaji Wambari amesema, Husna anapaswa kutoa ushahidi uliompa ushindi na kuagiza msimamizi wa uchaguzi huo kutoa ushahidi uliopelekea kumtangaze Husna Mwilima kama mshindi wajimbo hilo.
Baada ya kauli hiyo, Jaji Wambari ameahirisha kesi hiyo na kuagiza kusikilizwa tena Mei 3 mwaka huu.
Awali, Kafulila alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ambapo mahakama iliamuru chini ya Jaji Wambari kuwasilishwa fomu halisi za Matokeo ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kafulila alikubali na akaiomba mahakama kuiamrisha NEC kuwasilisha fomu hizo mahakamani ili ziweze kupitiwa kwa kulinganishwa na fomu alizowasilisha mahakamani na kupelekea Kenned Fungamtama, Wakili wa Serikali kupinga ombi hilo hapo awali.
Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, Kafulila alidai ndiye mshindi halali wa kiti cha ubunge jimboni hapo lakini Msimamizi wa Uchaguzi alimtangaza Husna kuwa mshindi kutoka CCM badala yake.
Post a Comment