Akizungumza
kwenye hafla ya makabidhiano ya mashuka hayo, Mwenyekiti wa SACCOS
hiyo, Bi Somoe Ismail Nguhwe, ameeleza kuwa msaada huo umelenga
kuisaidia hospitali hiyo ya rufaa kukidhi mahitaji ya mashuka ili
Kupunguza Tatizo lililopo.
Aidha,
Bi Nguhwe alisema kuwa Chama hicho cha wafanyakazi wa Tanesco
wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa hospitali na vituo vingi vya
afya nchini vinakabiliwa na uhaba wa mashuka pamoja na vifaa tiba
mbalimbali.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Saccos Hiyo mkoa wa Lindi, Mohamed Chembe
akimkaribisha Mwenyekiti wake wa Taifa Kukabidhi Msaada Huo alibainisha
Kuwa fedha zinazotumika kununulia mashuka ya misaada, zinatokana na
faida ambayo SACCOS inapata baada ya mahesabu ya mwaka kukaguliwa na
kutoa gharama na matumizi yote.
Akitoa shukurani baada ya Kukabidhiwa Msaada huo, Muuguzi Kiongozi wa
Wodi ya Akina mama na Magonjwa Mchanganyiko Bi Magdalena Mmuni
aliishukuru saccos ya Tanesco na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa
mashirika mbalimbali na wadau wa sekta ya afya kuiga hatua
iliyochukuliwa na saccos ya Tanesco ili kuzipunguzia hospitali makali ya
gharama za uendeshaji.
Sambamba na Utoaji wa Msaada Huo wa Mashuka 150 Baadhi ya wafanyakazi
wa Tanesco pia walipata Fursa ya Kuona wagonjwa Mbalimbali waliolazwa
katika Hospital Hiyo.
Post a Comment