0

Mkuu wa wilaya ya Liwale Bw.Ephraim Mmbaga aliyevaa nguo nyeusi akiwa hospitali ya misheni Ndanda na alipotembelea eneo la tukio.
Baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya misheni ya Ndanda wakiwa wanaendelea vizuri
Mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Bw. Ephraim Mmbaga jana alienda Ndanda katika Hospitali ya misheni ya Ndanda kuwajulia hali na kuwapa pole majeruhi wa ajari ya basi dogo la Halifa Family iliyotokea jumapili  april 10 majira ya asubuhi katika maeneo ya Daraja ya Nangoo-Ndanda na kufika eneo la tukio na kujionea hali iliyotokea.

Basi la Halifa Family hufanya safari zake kutoka Wilayani Liwale mkoani Lindi kwenda Mkoani Mtwara,siku ya jumapili april 10 basi hilo lilikuwa linatokea mkoani Mtwara kwenda wilayani Liwale lilipofika katika maeneo ya kijiji cha Nangoo maeneo ya Darajani liliacha njia na kupinduka. 

Mganga mfawidhi DR Crispin Sapuli alisema katika hospitali yake amepokea majeruhi 21,Katika ajari hiyo iliyotokea april 10 imepelekea kutokea kwa kifo cha Dr. Hamisi Ngole ambaye alikuwa anafanya kazi wa Halmashauri ya wilaya ya Liwale mkoani Lindi katika Hospitali ya Liwale, huku majeruhi wengine walipelekwa katika hospitali ya misheni ya Ndanda mkoani Mtwara kwa  kupatiwa matibabu.

 Pia Mbunge wa jimbo la Liwale,mh.Zuberi Kuchauka nae walienda hospitalini hapo kuwajulia hali na kuwapa pole majeruhi  na alisema majeruhi wawili Ally Ligai na mama Migomba wanatakiwa kupelekwa katika hospitali ya Muhimbili kwa matibu zaidi na majeruhi wengine wataendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo ya misheni ya Ndanda.

Mganga mfawidhi DR Crispin Sapuli alisema watoto wawili Baraka Mayunga ambaye yuko kwenye chumba cha watu mahututi kwa ajili ya uangalizi wa karibu na madaktari na Hawa Charles ambaye anaendelea kupata matibabu.

Aliwataja majeruhi wengine kuwa Sikudhani Mbega ambaye amefunjika mkuu wa kulia Idaya Chikawe. Ally Ligai Abedi mkopora ,Seif figera ,Devid Deotatus,Hasani Mohamedi, Saidi Abdala kimbunga,Mustapha Salimu, Hamisi Ngole ambaye alifariki kabla hajapata matibabu,Aliongeza kuwa wengine Asumta Migomba, Malisela Libena , Fatuma simon, Alfosa Imamuel , Salome Tayari, Prakisda Temba.

                       >>>kuangalia picha za kwenye tukio bofya hapa

Post a Comment

 
Top