0
 mgeni rasmi bwana Wilson Nyamanga akifuatilia risara ya chama cha bodaboda kwa umakini sana
 Afisa maendeleo ya jamii wilayani Liwale bibi Mary Ding'ohi akifafanua jambo
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale Mohamedi Mtesa akiwaeleza jambo wanachama wa bodaboda hii leo kwenye ofisi za bodaboda mjini Liwale
 Katibu tawala wilaya ya Liwale mkoani Lindi bwana Wilson Nyamanga akikabidhi pikipiki kwa mwanachama wa bodaboda
 Mgeni rasmi akikabidhi pikipiki kwa mwanacha hii leo maeneo ya ofisi za chama cha bodaboda
  Mgeni rasmi akikabidhi pikipiki kwa mwanacha  maeneo ya ofisi za chama cha bodaboda

MAKALA

Na Mwandae Mchungulike,Liwale
Namo februari 24 mwaka huu Chama cha waendesha bodaboda wilayani liwale mkoani lindi chatoa mikopo ya pikipiki kwa wanachama wake wapatao 62 zenye thamani ya shilingi 92,000,000.

Chama hicho kilipata mkopo wa pikipiki 20 zenye thamani ya shilingi 35,000.000 kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa Wilaya na kuweza kukopeshwa kwa mwanachama mmoja mmoja na kupitia umoja wao chama kiliweza kupata pikipiki 42 na kuweza kufikia ya jumla ya pikipiki 62.
 wamekabidhi pikipiki mbili kwa wanachama wawili zenye thamani ya shilingi 4,400,000/= na kukabidhi kwa mwanachama mmoja bati zenye thamani ya shilingi 2,000,00/= jumla ni 6,400,000/= na wameweza kufanya marejesho ya shilingi 6,325,000/=.
Katika hotuba yake katibu wa chama hicho ndugu Haji Mtutuma alisema chama cha bodaboda kilianzishwa mwezi mei 12 mwaka 2010 ikiwa na wanachama waanzishi 65 na kuweza kupata hati ya utambulisho kutoka idara ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Liwale mnamo januari 8 mwaka 2014.
Kwa sasa chama kina jumla ya wanachama 300 wenye sifa na vigezo vinavyokidhi mahitaji ya katiba na vigezo vinavyotumika kumkopesha mwanachama ni awe mwanachama hai na awe na kiwango cha hisa cha mwanachama.
Pamoja na mafanikio hayo yaliyopatikana zipo changamoto zinazowakwamisha kushindwa kutekeleza malengo yao ,changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa fedha za kuendesha ujenzi wa ofisi  pamoja na uwepo wa mtaji mdogo ambao unakosesha kuwakopesha pikipiki wanachama wengi kwa wakti mmoja.
Akikabidhi pikipiki hizo  mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya  bwana Wilsoni Nyamanga ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya liwale amewataka waendesha pikipiki hao kuwa na umoja kwani katika umoja huo kutasaidia kutatua  changamoto mbalimbali.
katika umoja wenu imekuwa ni chanzo cha ajira na tunatambua  wengi wenu ameepuka kujihusisha na vitendo viovyu vya kunyang’anya na kukaba pia sisi kama watu wa ulinzi na usalama kwetu ni faraja na kama serikali tumewatambua  kama wadau wa maendeleo”alisema Nyamanga.
Hata hivyo katibu tawala huyo amewasisitizia kuzingatia sheria na taratibu walizojiwekea katika katiba yao na kufanya maamuzi yanayoendana na malengo yao kwa kutaka kuwepo kwa viongozi bora na wa demokrasia ambayo mambo yote yanayofanyika yanakuwa ya wazi na shirikishi kwa kupeana taarifa mbalimbali na kuweza kuweka malengo makubwa na kuweka malengo yanayotekelezwa kwa kikomo.
Mmoja wa wanachama waliokabidhiwa pikipiki hizo leo Rajabu Kyula alisema amejisikia furaha sana kukabidhiwa pikpiki kwani mwanzoni alikuwa na pikipiki ya Bosi na sasa imekuwa mwokozi kwani sasa malengo yake yatakuwa yametimia na ataweza kukuza kipata chake pia amewashauri watu wengine kuweza kujiunga na chama hicho waweze kunufaika na mpango huo wa kukopeshana pikipiki.
Pia Idi Rashidi alisema amejiskia vizuri kukabidhiwa pikipiki na amewashauri watu wengine kujiunga na chama cha bodaboda kwani chama hicho kimekuwa mkombozi wa vijana wengi hapa wilayani.
 Mwenyekiti wa chama hicho Rafii Likochelo alisema amewawezeshaa wanachama wake kuwakabidhi pikipiki na bati na kwa msaada huu imewawezesha zaidi ya familia ya watu wanne watanufaika na mpango huu kwa wale waliojiunga na jitihadi zaidi ya kutafuta mkopo wa zaidi ya pikipiki 30 au 50 Kwa banki ya CRDB zinafanyika na hatua mzuri imefikia ya kukopeshwa  kwa lengo la kuwapatia wanachama wengi kuweza kupata mkopo kwa wale wanachama hai ambao wanalipa ada ya wanachama kwa mujibu wa katiba.
        
USIKOSE KUSOMA MAKALA ZINGINE ZA KAZI YA  VIJANA NA CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO KUTOKA WILAYA YA LIWALE MKOANI LINDI  

Post a Comment

 
Top