Licha ya kutupwa nje ya michuano ya klabu bingwa Afrika, kikosi cha Yanga kimepokelewa kishujaa na mashabiki wake waliokuwa wakiwasubiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius K. Nyerere, Dar es Salaa.
Kikosi cha Yanga kimeingia Bongo mchana wa leo April 22 kikitokea Misri ambako kilikuwa kinacheza mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly na mchezo huo kumalizika kwa Yanga kufungwa magoli 2-1 na kuondoshwa kwenye michuano hiyo.
Yanga walionesha kiwango cha juu kwenye mchezo huo kitu ambacho kimewafanya mashabiki wengi kwenda kuwalaki uwanja wa ndege wakati wakirejea.
Angalia picha zaidi kuona jinsi mashabiki wa Yanga walivyowatia moyo wachezaji wao licha ya kutupwa nje ya michuano ya klabu bingwa Afrika na kuangukia kwenye kombe la shirikisho Afrika.








Post a Comment