Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku
wafanyakazi wake ''Kuchati'' katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu
katika muda wa saa za kazi.
Waziri wa
Wizara hiyo Makame Mbarawa amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi,
kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii pamoja
na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na
maendeleo.
Ameongeza
kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila
ya kuonewa haya, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na
bidii ya kazi na weledi.
Lakini
hata hivyo, marufuku hiyo itaweza kufanikiwa?, kutokana na ukubwa wa
matumizi ya mtandao, huku walengwa wakiona wananufaika nayo.
Kutokana
na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, watu wengi
hususan vijana wamekuwa wakitumia muda mwingi katika mitandao ya
kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata
taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza.
Nchini
Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku
za hivi karibuni, hususan kupitia mitandao ya WhatsApp, Facebook,
Twitter na blogi mbalimbali.
Post a Comment