Waziri
Mkuu, Kassimu Majaliwa leo anatarajia kuanza ziara ya siku 14 katika
mikoa ya Kanda Ziwa kukagua shughuli na miradi ya maendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema Waziri Mkuu anayetarajiwa
kufika Mwanza saa nane mchana, atatembelea mikoa ya Simiyu, Kigoma,
Geita na Kagera.
“Ingawa
hakuna ratiba ya kutembelea eneo lolote mkoani Mwanza, tumejipanga kila
idara endapo atafanya ziara ya kushtukiza, tuko tayari,” alisema.
Wakati
huohuo; Mulongo alisema mke wa Rais, Janet Magufuli anatarajiwa
kutembelea Kituo cha Kulea Wazee Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi.
“Ziara hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8, kila mwaka,” alisema Mulongo

Post a Comment